Nini maana ya maendeleo ya Afya kwa upande wako...

Maendeleo ya Afya sio kwa kuwa na Mashine bora za kisasa, madawa bora au kuongezeka kwa vituo vya Afya.

Maendeleo bora ya Afya ni wewe kubadili mwenendo wa maisha yako, kula vizuri, kunywa kilichobora na kushughulisha mwili ili kuwa na maisha bora, nikuhabarishe kwamba... "Kutofanya kazi au Kutofanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku au dakika 150 kwa wiki inaweza kuwa sababu kubwa ambayo itakusababishia kupata au kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa yasiyo ambukizwa kama vile kisukari, shinikizo la damu au kiharusi katika maisha yako.''

Jivunie kuwa na Afya Njema.

Uwe na Asubuhi Njema

Comments