Makala iliyopita tulizungumzia mambo yakufanya ili umsaidie mtoto kujengeka kisaikolojia ili aachane na tabia ya kukojoa kitandani, natumai umefanyia kazi mambo hayo na leo nakuonesha kwanza njia asili tatu za kumsaidia mwanao kama bado anaendelea kukojoa kitandani.
Karibu sana,
01: Asali mbichi
Watoto wengi wanapenda ladha tamu ya asali na hivyo ni rahisi kutumika kwao kama dawa.
Mpe mtoto kijiko kidogo kimoja cha chai cha asali mbichi kila anapoenda kulala kila siku mpaka atakapopona. Unaweza pia kuchanganya na maziwa fresh wakati wa chai ya asubuhi itamsaidia kuimarisha kibofu na Afya.
02: Siki ya tufaa (Apple Cider Vinegar)
Siki ya tufaa husaidia kuweka sawa usawa wa asidi na alkaline mwilini (body’s Ph) na hivyo kupunguza asidi iliyozidi katika mwili kitu ambacho kinaweza kuwa ni moja ya sababu za tatizo la mtoto kukojoa kitandani.
Siki ya tufaa pia husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini pia hutibu tatizo la kufunga choo vitu vingine ambavyo husababisha tatizo la kukojoa kitandani.
~Mimina vijiko viwili vya chai vya siki ya tufaa ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya kunywa na umpe mtoto anywe kutwa mara 1 kila siku, unaweza pia kuongeza asali kidogo ndani yake kupata ladha.
Vizuri akinywa wakati wa kula chakula cha mchana au cha jioni.
03: Mbegu za Mharadali (Mustard Seeds)
Dawa nyingine nzuri kwa tatizo la kukojoa kitandani ni mbegu za mharadali. Ni dawa nzuri pia kwa wale wenye tatizo la U.T.I (yutiai).
Weka nusu kijiko kidogo cha chai cha mbegu za mharadali au unga wa mbegu hizi ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha maziwa fresh asubuhi na umpe mtoto anywe kinywaji hiki lisaa limoja kabla ya kwenda kulala kila siku mpaka amepona.
Mambo ya muhimu kuzingatia ili ufanikiwe na dawa hizi:
• Wasiwasi na mfadhaiko (stress) huweza kuongeza ukubwa wa tatizo. Hivyo badala ya kumkalipia au kumdhalilisha kila siku mtoto muonyeshe upendo na uwe tayari kumsaidia polepole mpaka anapona tofauti na hapo tegemea tatizo kutokuisha kwa haraka.
• Mhimize mtoto kwenda kukojoa kabla ya kwenda kulala kila siku
• Hakikisha kuna taa au mwanga wa kutosha njia ya kuelekea chooni, wakati mwingine mtoto akiona giza anaogopa kwenda chooni hasa kama choo kipo mbali na anapolala hasa kwenye nyumba zetu hizi za uswahilini 😆😆
• Mpe zawadi yoyote ndogo kila siku anapofanikiwa kuamka salama bila kukojoa kitandani, hii itamuongezea nguvu na moyo zaidi wa kujidhibiti zaidi na tatizo lake.
• Dhibiti matumizi ya juisi hasa juisi zenye sukari nyingi na za dukani nyakati za jioni.
• Epuka vinywaji vyenye kaffeina kama vile chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi, malta, energy drinks zote na vingine vyote vyenye kaffeina ikiwemo chokoleti
• Tibu tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.
• Tumia karatasi linalozuia maji kupenya kwenye godoro moja kwa moja ili
kupunguza harufu mbaya chumbani na usumbufu usio wa lazima.
• Weka alamu muda ule unaona mara nyingi mtoto ndiyo hujikojolea, weka saa yenye kengele (alarm) muda huo ili aweze kushtuka kabla na aende chooni.
Tatizo la kukojoa kitandani si tatizo linaloweza kutibika kwa haraka haraka ndani ya siku 2 au 3. Kuwa mvumilivu na mpole, walau jaribu tiba kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo na usikate tama haraka.
Nitaonesha njia nyingine mbadala za kufanya, natumai mwanao pia atafurahia mabadiliko yake.
Kwa usaidizi binafsi PIGA au Tuandikie ujumbe wako kwenda WhatsApp no. +255769321005
Tupo kwa ajili yako wewe mwenye changamoto ya
•Miguu/mikono kufa ganzi na kuwaka moto (neuropathy)
•Baridi Yabisi (Arthritis)
•Bawasiri/Kupata choo kigumu, maumivu na kijinyama kutoke nje wakati wa haja kubwa
•Ngiri/Hernia
•Matatizo ya uzazi, hedhi na Ugumba kwa jinsia zote
•Tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa
•Kutibu athari za punyeto
•Kisukari (Aina zote)
•Presha (Aina zote)
•Pumu/Asthma
•Lipoma (Uvimbe unaojitokeza katika mwili halafu hauna maumivu yoyote)
•U.T.I Sugu, Fangasi ukeni, Harufu mbaya kwenye kinywa, ukeni na kadhalika.
Zipo TIBA ASILI ZENYE KUTIBU MAGONJWA HAYO,
Tunapatikana Ubungo Mawasiliano mkabala na simu2000
Comments
Post a Comment