Utofauti Uliopo Kati Ya Dawa Asili au Tiba Lishe na Dawa za Kisasa

IJUE TOFAUTI ILIYOPO KATI YA DAWA ZA MITISHAMBA (Herbalism) na DAWA ZA HOSPITALINI (Drugs).

Dawa ni nini sasa?
Maana ziko nyingi sana lakini nikupe hii, dawa ni kitu ambacho kina uwezo wa kusaidiana na mwili kuondoa maradhi yaliyoibuka kwa kushughulika na fiziojia ya mwili.
Tunatarajia dawa yoyote iwe na kemikali ndani yake yenye uwezo wa kutibu (active ingredients). Kwa hiyo sio za asili au za kisasa dawa zote zina kemikali!

Kwa Kemikali ni nini et!!?

•Kulingana na Wikipedia kemikali ni kitu chochote chenye muundo kamili kikemia na kinasifa inayokitambulisha.

Hata vyanzo vingine vya taarifa huunga mkono hili.
Kumbe vitu vingi sana ni kemikali mfano, Tunavuta hewa ya oksijeni ni kemikali, chakula tunachokula kuna virutubisho kama kabohaidreti, vitamin, chumvichumvi, protini na mafuta vyote hivi ni kemikali.
Kumbe hata ukinywa maji nayo ni kemikali, kwa kweli kemikali kumbe ni muhimu sana!

Maana ziko nyingi sana lakini ni
Kumbuka sio kila kemikali ni mbaya kwenye mwili japo zipo ambazo ni hatari hata kama zikiwa kwa kiwango kidogo sana mfano zebaki (mercury), aluminum n.k. Lakini pia zile ambazo ni salama zikiwa kwa kiwango kikubwa sana inakuwa SUMU!

Kwa mfano, vitamin A ni muhimu sana mwilini lakini inaweza kuwa sumu kama itakuwepo nyingi kupita kiasi. Pia madini ya chokaa (calcium) ni muhimu sana sana kwa ajili ya afya ya mifupa, misuli na utendaji kazi wa mfumo wa fahamu lakini kama ikiingizwa mwilini kwa wingi kupita kiasi (zaidi ya 2000mg kwa siku) ni SUMU na utapata shida lukuki za kiafya.

NAJUA HAPA NIMEKUCHANGANYA KWA KIASI FULANI ila usihofu mbeleni utaelewa zaidi:
 endelea kusoma!



_______Sasa kwa kuwa tumegundua kuwa dawa zote ni kemikali, kuna tofauti gani kati ya dawa za asili na zile za kisasa na je ni zipi zipo salama zaidi?

TOFAUTI ZILIZOPO

1. MAANA ZAKE

A/ Dawa za kisasa ni zile ambazo zinazalishwa viwandani kwa kutumia vyanzo visivyo vya asili au kunyofoa baadhi ya kemikali muhimu (active ingredients) kutoka vitu vya asili na kuziweka pamoja kwa wingi katika ujazo mdogo
(concentrated) na hapo ndipo tunapopata jina la
SUMU.

Dawa za kisasa zimetengenezwa kwa misingi ili kufanya kazi na mfumo wa matibabu wa kisasa ambao una kanuni hizi:
a) kutumia sumu ili kutibu magonjwa kwa haraka (quick recovery)

b) kama kiungo kimeathirika sana kikatwe

c) kwa ajili ya biashara (money related)

B/ Dawa za asili ni zile ambazo zimetokana na mimea, mazao ya wanyama, na vitu vingine vinavyopatikana kwa asili kwenye mazingira yetu au vijapoandaliwa kiwandani kwa maana ya kufungashwa vizuri kwa matumizi. Vitu hivi vina kemikali nyingi sana kwa kiwango kidogo kidogo.

Vina kemikali tiba (active ingredients) na kemikali zingine kwa ajili ya kuulinda mwili na kusaidia mwili kufanya kazi yake vema ili kujipatia afya njema mfano Kemikali za mimea
(phytochemicals), vitamins, madini, protin n.k

Dawa hizi zinafanya kazi pamoja na mfumo wa tiba ya asili na tiba mbadala ambao hizi ndizo kanuni zake:
a) kutibu maradhi ya mwili kwa kuusaidia mwili kujitibu wenyewe

b) kama kiungo kimeathirika sana kisaidiwe kujiponya na sio kukikata.

c) hujali uhai wa watu kwanza kwa sababu huwaelekeza watu kutumia vitu vinavyowazunguka kujitibu na sio kutegemea vilivyotengenezwa ili wanunue.

2. KIWANGO CHA KEMIKALI
Licha ya kuwa dawa zote zina kemikali, dawa za kisasa zina kemikali chache kwa kiwango kikubwa sana (concentrated) ambazo nyingi kati yazo zimetolewa kwenye mimea na viumbe wengine.
Na hivyo kwa kuwa kemikali hizi zipo kwa wingi sana (concentrated) zinapanda daraja na kuitwa
SUMU.
Ndio maana zinaweza kutibu kwa haraka.
Changamoto:
Sumu iliyotumika kutibu inatakiwa itoke nje ya mwili. Ini, figo, ngozi na viungo vingine hufanya kazi ya kuondoa sumu hiyo. Lakini kutokana na kwamba sumu hiyo IPO kwa kiwango kikubwa viungo hivi haviwezi kuitoa yote na hivyo sumu inabakia mwilini na kusababisha ugonjwa mwingine. Itakupasa kutumia dawa za kupunguza sumu mwilini (dexofication)

Zaidi, dawa za kisasa hazina kemikali zingine rafiki ya mwili kama phytochemicals, vitamin, madini n.k kwa ajili ya kusaidia mwili kujipatia afya njema.

Dawa za asili hazina sumu, kwa sababu kemikali tiba (active ingredients) IPO kwa kiwango kidogo kiasi ambacho mwili unaweza kukitoa nje baada ya matumizi.
Pia zimeambatana na marafiki wengine wa mwili kama phytochemicals, vitamin na madini ili kuusaidia mwili kufanya kazi zake vilivyo na kuleta ustawi wa afya. Pia viambata hivi husaidia hata hivyo viungo vinavyohusika na kutoa sumu vifanye kazi vema.

Changamoto:
Licha ya kwamba tiba yake huleta afya ya muda mrefu, huchukua muda mrefu kutibu ugonjwa pia.
 Mfano Badala ya kutumia siku 3 dozi ya malaria kwa dawa za kisasa inaweza kukuchukua hata siku 14 kwa dawa za asili.
Wahenga wapo wengi, wengine wanasema "haraka haraka haina Baraka' na wengine "ngoja ngoja yaumiza matumbo" sasa ni wewe kuchagua Mhenga yupi unayempenda ...
Ila Mimi nasema "kawia ufike".

3. MADHARA YA BAADAE [Side Effects]
Hivi umewahi kusikia madhara ya kula ugali? Kula nanasi je? Au madhara ya kula kitunguu saumu..? Bila shaka hakuna. Ndivyo ilivyo kwa dawa za asili kwa sababu hazina sumu.
Haya umewahi kusikia madhara ya panadol? Vipi kuhusu asprin na dawa za kupambana na tindikali ya tumbo..? Madhara yapo ya kujichotea wala si kutafuta na tochi. Ni rahisi tu kwa sababu dawa hizi zina sumu!

Hapa ndio penye busara binafsi..
Tunashukuru sana mfumo wa tiba ya kisasa imetuletea vifaa ili kubaini magonjwa kwa urahisi.. Ila inapokuja suala la kutumia dawa kuwa mjanja kama hua na mwerevu kama nyoka.

Lengo sio kukataza Dawa za Hospital zisitumike, La Hasha. Ni kukuweka wazi ili uishi kwa tahadhari juu ya Afya Yako, kuitunza na kuihudumia kwani ndio mtaji wako wa kwanza katika hizi mbio zetu za kutafuta maisha bora.

Kula vizuri, upe mwili mazoezi, ishi kwa tabasamu, ishi kwa kuifuata misingi ya Upendo na KWA AJILI YA KUSUDI LA MWENYEZI MUNGU hakika utaiona Dunia Tamu.

Mwenyezi Awabariki

Comments