MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUFAHAMU KUHUSU HOMONI, HEDHI NA KUPATA UJAUZITO

Utangulizi

HATUA AMBAZO MWILI HUPITIA ILI WEWE UPATE HEDHI YENYE MPANGILIO na  UJAUZITO

 


1: Hatua ya kwanza, kwa msaada wa homoni ya Follicle na Oestrogen yai hutengenezwa na kukomaa katika vifuko vya mayai (ovari)

2. Moja kati ya ovari zako huachia yai lililokomaa kwa ajili ya kwenda kurutubishwa na mbegu za mwanaume

3. Yai hili lililokomaa linatakiwa kusafirishwa kutoka katika ovari mpaka kwenye mrija wa uzazi (fallopian tube)

4. Mbegu za mwanaume (shahawa) husafiri kuanzia kwenye mlango wa uke (cervix), kupitia tumbo la uzazi (uterus) hadi kwenye mrija wa uzazi, kulifikia yai la mwanamke lililopevushwa kisha hulirutubisha (kutengeneza kijusi)

5. Yai lililorutubishwa husafiri kupitia mrija wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi na kujishikiza na kuanza kukua siku hadi siku na huo ndio mwanzo wa safari ya ujauzito

Iwapo yai la mwanamke halijarutubishwa katika siku za uzazi (danger days) baada ya siku 14 hutolewa nje kama uchafu ambayo ndio damu ya hedhi tunayoizungumzia

 Katika hatua zote hizo hapo juu tumeona vitu muhimu vinavyohusishwa ili kukamilisha mambo yote  ikiwepo HOMONI, MIRIJA YA UZAZI, OVARI (Vifuko Vya Mayai Ya Mwanamke), Fuko La Uzazi (Uterus) na MBEGU ZA MWANAUME....

hivyo ikitokea kuna tatizo katika moja ya vitu hivyo, kupata hedhi au ujauzito kwa wakati huwa ni jambo gumu, ndio maana umejiunga katika jukwaa hili kupata ufumbuzi wa haya mambo ili ukomboe muda, gharama na sintofahamu zote kuhusu uzazi....

Nimekuwa nikikutana na wanawake kama wewe waliokaa katika ndoa zaidi ya mwaka mmoja, mitatu na wengine mpaka miaka 7 bila kupata watoto ila baada ya kuwasilikiliza na kuwapa maelekezo juu ya mambo muhimu ya kuzingatia hivi sasa ni wajawazito na wengine wamejifungua tayari.

Ni wewe kuwa makini na kuchukua hatua, nina uhakika ndani ya siku 30 ni lazima uje na mrejesho mzuri tu

Ili tuweze kufanikisha ndoto yetu ya hedhi salama na kupata ujauzito ni lazima HOMONI zetu ziwe katika mpangilio ulio mzuri, hiyo ni lazima

Labda unajiuliza, Kwani homoni ni nini na ni kwa nini bila homoni ndoto zetu za uzazi huonekana kukwama?

Kwa sababu ya kukomboa muda itabidi nifafanue kwa ufupi sana ili tujue umuhimu wa vitu hivi, ili siku daktari anakwambia una tatizo la Mvurugiko wa Homoni / Hormone Imbalance ujue anamaanisha kitu gani...

Karibu tujifunze wote.

👇🏾

Homoni ni kichocheo ambacho hutengenezwa na tezi mbalimbali mwilini na kusafirishwa na damu kwenda sehemu inapohitajika mwilini ili kutenda shughuli maalum.

 Homoni zipo nyingi mwilini na kila homoni huwa na kazi yake maalumu.

Homoni tunasema ni “Kichocheo” kwa sababu madhumuni ya kutengenezwa kwa homoni ni kwenda kuchochea tendo fulani la kibaolojia litokee mwilini.

Mfano: Homoni ya kike estrogen hutengenezwa na tezi iitwayo ovari na huenda kuchochea mambo mbalimbali kwa mwanamke kama kubarehe kwa mwanamke (Kuota matiti, Ngozi laini, nyoga kuongezeka, sauti nyororo).

Homoni zipo aina nyingi, kuna homoni za uzazi, usagaji chakula, zinazo ratibu matumizi ya wanga, mafuta na protein n.k katika somo letu hili tunajifunza homoni za uzazi kwa mwanamke pekee.

Homoni ambazo zinachochea matukio mbalimbali ya uzazi kwa mwanamke ni Oestrogen, Progesterone, Prolactin, Follicle stimulating hormone (FSH), Luteinizing hormone (LH), na Testosterone.

Homoni hizi huwa zinatengenezwa na ovari kwa mwanamke na kuratibiwa na (Anterior Pituitary Gland) tezi ambayo huhakikisha homoni zinabalansi isitokee homoni baadhi ziko juu na nyingine ziko chini.

Umuhimu wa kila homoni na madhara yake iwapo itapanda au kushuka sana.

Homoni ya Estrogen

👇🏾

~Homoni hii huchochea matendo yote wakati wa kubalehe kama Kuota matiti, Ngozi kuwa laini, sauti nyororo, nyoga kuongezeka n.k

~Hujenga ukuta wa kizazi ili mimba ije ijishikize kwenye ukuta mnene.

Homoni ya Progesterone

👇🏾

~Hutengenezwa na tezi ya dharura (corpus luteum) pale ambapo yai limetoka katika ovari

~Kazi yake kubwa ni kulea mimba, inaongezeka sana baada ya siku ya kupevuka kwa yai na baada ya mimba kutungwa.

~Endapo mimba isipotungwa homoni hii inayoshikilia ukuta usibomoke hushuka kiwango chake na ndipo inawezesha ukuta kuporomoka kwa kutoa uchafu (damu ya hedhi) ili kwamba ukuta mwingine ujengwe kwa ajili mzunguko wa hedhi ujao

~Pia hukuza matiti wakati una mimba na kuendelea kufanya ukuta wa kizazi uwe imara ili mimba isichoropoke kabla ya miezi tisa

Homoni Ya Prolactin

👇🏾

Hii ni homoni ambayo hupanda sana wakati una mimba na wakati unakaribia kujifungua

~Hutengeneza maziwa yakutosha ili uweze kunyonyesha

~Huwa ina mkinga mama asipate mimba mapema akiwa bado ananyonyesha. Ukiwa unanyonyesha homoni hii huwa nyingi na huzuia upevushaji wa mayai. Ila unashauriwa baada ya wiki sita tangu umejifungua kuwa makini maana kwa unyonyeshaji wa nadra kwa wanawake wengi unasababisha prolactin kutokuwa katika kiwango toshelevu kuzuia upevushaji wa mayai.

●Testosterone

Tunaita hii ni “homoni ya kiume” kwa sababu huwa ndio imetawala (inajionesha kuwa juu) kwa mwanaume kuliko homoni zingine. Lakini wanawake pia huwa wana hii homoni katika kiwango kidogo sana. Wao homoni inayotawala ni oestrogen.

~Homoni hii inasaidia sana uhifadhi wa mafuta mwilini, pia inasaidia katika utumiaji wa vyakula vya mafuta, protini na wanga, pia inasaidia sana kutengeneza misuli ya mwili wako. Hivyo ni ya muhimu pia kwa mwanamke japo sio muhimu sana 

Follicle Stimulating Hormone (FSH)

👇🏾

Hii ni homoni ambayo inakomaza mayai, na huanza kupanda kwenye damu siku ya kwanza tu umeanza kuingia hedhi.
    Yenyewe inaanza kuandaa yai ambalo litapevuka siku ya hatari katika mzunguko wako.

Homoni ya Lutein (LH

Ni homoni ambayo husaidia yai liweze kutoka kwenye ovari, liende kwenye mirija ya uzazi kwa ajili ya urutubishaji.

Kuvurugika kwa homoni maana yake ni nini?
       
Maana yake ni kwamba homoni zako haziko katika uwiano unaotakiwa na zinasababisha kwa namna moja au nyingine mzunguko wako wa hedhi unakuwa haueleweki na tatizo husababisha kutobeba mimba au mimba kutoka mapema kabla ya kufikisha mwezi mmoja.

Tazama mifano hii hapa chini

Endapo homoni ya estrogen ikiwa juu sana inaweza kukuhatarisha kiasi cha kupata

~Shinikizo la juu la damu (presha kupanda)

~Hapa ndipo unakuwa unasikia hupumui vizuri, mapigo ya moyo yanaenda mbio, kuhisi joto jingi au kutoka jasho sana mara nyingi inapofika usiku, ukiona dalili hizi na hedhi yako haieleweki basi elewa homoni hii ipo juu sana kuliko inavyohitajika.

Pili ongezeko la homoni ya oestrogen husababisha uwepo wa vivimbe katika fuko la uzazi kitaalam huitwa (fibroids)

Homoni ya progesterone inapokuwa chini sana inaweza kusababisha yafuatayo

~Mwanamke kupata maumivu makali sana ya tumbo wakati akiwa hedhi

~Kupata hedhi yenye kuambatana na kutokwa na damu nyingi sana na kwa muda mrefu

~Mimba kuwa zinatoka, kila unapobeba mimba inatoka hata kabla haijamaliza miezi 3.

~Progestrone ikiwa juu hupelekea mwanamke kupata hedhi nyingi kupitiliza, unaweza kujikuta kwa mwezi unaingia mara mbili au zaidi

Homoni ya Prolactin ikiwa juu sana kwenye damu unaweza kupata matatizo yafuatayo kiafya

Kumbuka homoni hii inapanda unapokuwa una mimba na unanyonyesha tu. Lakini ukikuta ipo juu sana kwenye damu wakati hunyonyeshi na huna mimba kiafya inakuwa sio salama.

~Inaweza kusababisha matiti kuvimba, kujaa na kutoa maji au maziwa wakati huna mimba.

~Maziwa kujaa sana au kuuma kiasi unakuwa hutamani hata kuvaa nguo wala kushikwa chuchu

• Huwezi kubeba mimba kabisa kwa sababu prolactin ikiwa juu wakati huna mimba huenda kuzuia ovari zisikomaze mayai na zaidi mayai huwa hayapevuki

Homoni ya testosterone ikiwa juu kwa mwanamke unaweza kupata madhara yafuatayo kiafya;

~Kutopevusha mayai kila mzunguko wa hedhi inaweza kusababisha ukawa mgumba.

~Mayai yanakuwa hayapevuki na matokeo yake unapata uvimbe kwenye ovari tunaita “PolyCyst” au kwa kifupi Pcos. Ambapo cyst inaweza kuwa moja na kubwa au zinaweza kuwa nyingi “Polycysts”. Kwa hiyo unakuwa hatarini kupata uvimbe kwenye ovari.

~Kuota nywele sehemu ambazo mwanamke hutakiwi kuwa na nywele. Mfano ndevu kwa mwanamke, nywele kifuani n.k

~Hamu ya tendo la ndoa hupotea kwako inakuwa ni maumivu tu wakati wa tendo la ndoa.

~Kupata Damu ya utelezi na kukosa ute wa uzazi siku za uzazi (danger days)

Mpaka hapa umeweza kutambua ni homoni gani inakusumbua kulingana na dalili unazozipata?

MAMBO GANI HUVURUGA HOMONI ZA UZAZI

Kama tulivyoona hapo nyuma kuwa homoni ni kichocheo ambacho husafirishwa katika damu,  homoni uzalishwa na Ovary na Kuratibiwa na Tezi Ya Pituitary

Hivyo vitu vitatu endapo kimojawapo kitaharibiwa moja kwa moja homoni zetu huvurugika pia.

Baadhi ya vitu ambavyo vimekuwa vikivuruga homoni zetu za uzazi ni pamoja na;

MAGONJWA

Mfano

👉🏾Mtu mwenye matatizo ya Kisukari moja kwa moja ana uwezekano wa kupata matatizo ya homoni kuvurugika kwa sababu ya matatizo yake ya insulin kushindwa kuratibu kiwango cha sukari na wanga katika damu, kama una matatizo ya kisukari bila shaka utakuwa chini ya uangalizi wa madaktari... Kundi la watu wa kisukari sio kubwa kwa hapa Tanzania, wengi wetu homoni zetu zimevurugika kwa sababu ya;

•Matumizi ya Njia Za Kisasa Za Uzazi wa Mpango.

==> Ukiachana na propaganda za serikali na mambo ya uchumi umewahi kuwaza na kutafakari ni kwa nini haswa huwezi kubeba mimba ukiwa unatumia uzazi wa mpango?

Dhamira kuu ya njia za kisasa huwa ni kuua au kuharibu uwezo wa uzalishwaji wa vichocheo au homoni  za uzazi (progestrone oestrogen) ili mimba isifanikiwe kutungwa.

Kesi za mara kwa mara ambazo unaweza kuzisikia kwa wanaotumia au waliowahi kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango ni pamoja na..

~Hedhi kukosa kwa muda mrefu hata miezi miwili bila kuona damu ya hedhi au damu za hedhi kutoka kwa muda mrefu zaidi ya siku 10 hata wiki kadhaa damu haiachi kutoka matone

~Maumivu wakati wa hedhi au kuhisi muwasho na ute ute wenye uchafu hata baada ya hedhi kuisha

~Matiti kujaa sana kabla ya hedhi, kuhisi maumivu makali ili hii hutegemea na njia ipi ya kisasa anatumia au alitumia kupanga uzazi..... Nitaonesha baadhi hapa chini, kama ni mtumiaji utakuwa shahidi katika njia unayotumia au uliowahi kutumia.

•Sababu nyingine zinazovuruga homoni ni Maambukizi Katika Via Vya Uzazi

~Maambukizi ya Bakteria au Fangasi katika via vya uzazi huathiri mpangilio wa homoni, hii ni kwa sababu bakteria au fangasi huweza kusambaa kwenye fuko la uzazi, mirija ya uzazi na kushambulia fuko la mayai (ovari). Fangasi au bakteria wanaposhambulia husababisha ovary kuwa na vivimbe vidogo vidogo (ovarian cyst) jambo ambalo matokeo yake husababisha ovary kushindwa kuzalisha mayai ya mwanamke kwa wakati na kupelekea kukosa hedhi kwa wakati sahihi. Dalili nyinginezo zinazoweza kuonesha kuwa una mashambulizi ya bakteria au fangasi ni maumivu makali kwenye nyonga, maumivu ya pembeni mwa tumbo maeneo ya chini ya kitovu, mkojo kuwa mchafu au U.T.I sugu, Kutokwa na Uchafu Ukeni na kama umepima hospital unaweza kuambiwa una tatizo la P.I.D

Jambo jingine linalovuruguka homoni za mwanamke ni matumizi ya vidonge vya dharura vya kuharibu mimba kama P2, mesoprostol na kuharibu mimba mara kwa mara kwa njia za kumeza madawa makali.

•Kuwa na matatizo ya Uvimbe katika Fuko la Uzazi (Fibroid/Myoma)

Mwenye tatizo hili huwa na dalili km kutoka hedhi nyingi kupitiliza, unaweza kupata hedhi zaidi ya siku 7 au ikatoka mara mbili kwa mwezi

~Kuhisi km kitu kinacheza tumboni au km kimening'inia tumboni

~Tumbo kujaa

~Maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu n.k (tutajifunza haya kesho kutwa)

Ni jambo gani kati ya hayo niliyotaja umewahi kuyapitia, kuyatumia au unahisi ndio chanzo cha wewe kukosa mimba na hedhi kuvurugika..!?

Mambo Yenye Kusaidia Kutibu Tatizo La Mvurugiko wa Homoni (Hormones Imbalance)

Hapo awali tumeona umuhimu wa homoni na mchango wake katika kuhakikisha tunafanikisha ndoto zetu za hedhi salama na kupata ujauzito na baadhi ya dalili zake ambapo tumesema mwenye tatizo la homoni imbalansi huwa na dalili kama;

~Kuwa mkavu wa uke wakati wa kushiriki tendo la ndoa kiasi cha kupata maumivu makali wakati wa faragha...

- Kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka (hedhi kusimama / kurukaruka/ kupitiliza wiki au mwezi bila kuona bleed)

- Kukosa ute wa uzazi zikifika siku za hatari

- Kuhisi uvimbe au mjongeo wa vitu ndani ya tumbo

-Hedhi kutoka nyingi kupitiliza,/ kupata hedhi  yenye utelezi

- Kukosa hedhi kwa muda mrefu, na kutoa damu yenye nyama nyama au mabonge

-Mapigo ya moyo kwenda mbio, hasira za mara kwa mara, kuhisi joto sana haswa nyakati za usiku

- Kukosa kubeba mimba hata ushiriki tendo siku zote za mzunguko bado mimba hupati

-Kupata dalili za mimba kama matiti kujaa, kichefuchefu, kupitiliza hata siku lakini ukipima mimba hamna.

Hapa chini nimekushirikisha baadhi ya njia ambazo huwa nawashauri wanawake ambao wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili la homoni....

  Katika njia hizi  ichague mojawapo ambayo unaweza kuiandaa, fuatisha vipimo vyake na itakusaidia kukupa matokeo mazuri...

Njia ya Kwanza ni Kutumia ASALI Mbichi ya Nyuki Wadogo kwa kuchanganya na VIUNGO VYA MAPISHI.

~Hii ni njia ya asili ambayo huwasaidia haswa wale ambao mvurugiko wao wa homoni umesababishwa na uzito kuwa juu, mimba kuharibika au matumizi ya muda mrefu ya njia za uzazi wa mpango kama kijiti na sindano.

Mahitaji:

>Tangawizi kubwa nne (katakata ili iweze kusagika vyema kwenye blenda au twanga) kama ni unga basi iwe vijiko nane

>Vitunguu saumu glass moja (menya vizuri) kama ni unga iwe vijiko nane hadi kumi

>Mdalasini wa unga vijiko sita

>Asali mbichi PURE ya nyuki wadogo lita moja. [ikikosa ya nyuki wadogo unaweza kutumia asali ya nyuki wakubwa kama hausumbuliwi na vidonda vya tumbo, muhimu iwe asali mbichi]

 Maandalizi.

Chukua tangawizi na vitunguu saumu na usage kwenye blenda viwe laini kisha utaweka unga wa mdalasini na utaanza kumimina asali yako kidogo kidogo hadi iishe kisha itakuwa nzito sana hivyo utaanza kuongeza maji kidogo kidogo hadi nusu lita ya maji iishe kabisa kwa maana juisi yako itakuwa ujazo wa lita moja na nusu

>>Kama viambata vyote vitakuwa vya unga au umesaga kwa kinu, huna haja ya blenda, utaweka viambata vyote muhimu kwenye kifaa cha kukorogea iwe sufuria au kontena kisha utaanza kuweka asali na kumalizia na maji nusu lita ya maji ya kawaida.

•Matumizi ya dawa

>>Asubuhi utatumia nusu glass ya juisi hii, mchana na jioni hadi itakapoisha, mathalani itachukua siku tano kuimaliza, utaandaa nyingine tumia dawa hii mfululizo kwa siku 15 hadi 21.

Utapona vizuri, utajiskia mwepesi na utaanza kulifurahia tendo la ndoa bila ukavu...!!

02: Njia Ya Pili ni Dawa Nne Za MITISHAMBA

Njia ya pili ni kutumia dawa za mitishamba na huku ndipo mirejesho mingi inakuwa na majibu mazuri kwa wenye changamoto nyingi za uzazi yatokanayo na U.T.I sugu, Uzazi Wa Mpango,  Vivimbe n.k

Chukua Dawa Asili hizi nne katika ujazo unaolingana.

👇

Unga wa Mrehani [basil leaves powder] robo kilo

Unga wa habat sawda (black seed), robo kilo

Unga wa mbegu za uwatu (fenugreek) robo kilo na Unga wa mizizi ya Mkunde pori robo kilo.

MAANDALIZI

  Changanya kwa pamoja dawa hizi kwenye bakuli moja, uwe unatumia unga wa mchanganyiko wa dawa hizi kijiko kidogo kimoja kwenye chai, uji, au maji moto tumia mara tatu kwa siku, kwa wiki 3 mpk 4. Kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu utakuwa umefanikiwa kutatua hizi changamoto za homoni kuvurugika na kama ni kuhusu kupata mimba inakuwa rahisi sana

Haijalishi ni kwa muda gani umekuwa ukitafuta suluhu bila mafanikio, kama utaamua kuanza upya na kuchukua hatua, utaona matokeo mazuri, natumaini utanipa mrejesho wako pia kadri utavyokuwa unaendelea kutumia

Ili uweze kupata matokeo mapema itakuwa vyema kama utajitahidi kujiweka vizuri hata kwenye upande wa vyakula, kama tujuavyo kuwa unachokiingiza mwilini ndicho kina nguvu zaidi ya kukujenga au kukuharibu hivyo hakikisha unakula vile vyenye kuupa mwili afya njema zaidi

• Punguza (ikibidi acha) kula vyakula vya kukobolewa kama mkate mweupe, chapati, mandazi n.k kama unapenda sana ugali basi tumia dona, kama ni mkate tumia ile mikate ya brown ambavyo ngano yake huwa haikobolewi.

• Pendelea zaidi kula matunda kwa wingi mfano ndizi mbivu, papai, chungwa, embe, nanasi, karoti, tikiti, tango n.k (matunda utayopata kula) na mboga za kijani kwa sana tu. (matunda na mboga za kijani iwe sehemu ya mlo wako pia)

Kuna viungo vya chai / mapishi ambavyo nakushauri kuvipa kipaumbele zaidi mfano Iliki, Mdalasini, Tangawizi, Karafuu na  Binzari Ya Manjano
Ni viungo vizuri kwa kusafisha njia za mkojo, damu na kubalansi homoni iwe kwa mwanaume au mwanamke....

Ukizingatia Hayo Mambo Ndani Ya Mwezi Mmoja Hutokuwa na Tatizo la Homoni Kuvurugika Tena na Mimba Utapata Vizuri tu

  Kama una changamoto nyingi za uzazi zinazokusumbua, tumia

MIXED HERB POWDER

➡️Ni dawa asili ambayo inaondoa uchafu na fangasi kwenye kizazi

➡️inatoa uvimbe kwenye kizazi (fibroids) na vimbe kwenye fuko la mayai (ovarian cysts)

➡️ Inazibua mirija na kuondoa tatizo la mvurugiko wa homoni kama unakoswa hisia, ute, mimba hazinasi na hedhi haieleweki

Dozi hii unaipata kwa Tsh 66,000 tu

Wakazi wa Dar, tupo Machinga Complex na pia tunakuletea hadi ulipo FREE

Kwa mawasiliano zaidi tutafute 0757487684

Asili Yetu Afrika
Tunatimiza Ndoto Yako Ya Uzazi

Comments