Baadhi Ya Vyakula / Mimea Yenye Kukusaidia Kuongeza Uchungu




 


 Wakati ambapo hakuna utafiti tosha kuegemeza imani kuwa vyakula vinaweza anzisha uchungu wa uzazi, wanawake wengi wana uhakika kuwa kuna vyakula vilivyowasaidia kuanzisha uchungu wa uzazi. Hapa kuna baadhi ya vyakula vya kukusaidia kuanzisha uchungu wa uzazi kwa njia asili ambavyo wanawake wengi wamekiri kuwa vimewasaidia. Kwa hivyo ikiwa uko katika wiki zako za mwisho za ujauzito, na mtoto bado hajafika, hapa kuna baadhi ya vyakula vitakavyokusaidia sana.

• Nanasi

Kulingana na baadhi ya wanawake, kula mananasi ni njia nzuri ya kufuata. Lakini, hakuna utafiti wa kudhibitisha haya. Enzyme ya proteolytic iliyoko kwenye mananasi freshi, na bromelain inaweza legeza tishu inayo zunguka mlango wa uke na kusaidia kuanzisha uchungu kwa wanawake waliofikia wakati wa kujifungua.

•Papai

Papai za kijani ambazo hazijaiva vizuri, zina wingi wa enzyme ya papain. Majani ya mpapai yana latex inayofanya kazi sawa na prostaglandin na oxytocin na inaweza anzisha uchungu wa uzazi. Kadri papai linavyozidi kuiva, ndivyo papain inavyozidi kupungua. Unaweza kulimenya na kutafuna au kumenya kisha kusaga ili kutengeneza juisi yake

•Mafuta Ya Mnyonyo

Jamii zetu za kiafrika hapo kale njia hii imekuwa ikitumika kwa wanawake kuanzisha uchungu wa uzazi. Unaweza kuitumia matone kadhaa kwenye chai au juisi yako na wengine huweza kuyatumia kwa kumasaji 

•Zabibu

Zabibu ni vyanzo vizuri vya nishati kwa wanawake walio chelewa kujifungua kufuatia kiwango cha juu cha wanga. Na kufanya zabibu ziwe chanzo kizuri cha nishati inayo kusaidia kuwa na nishati tosha ya kujifungua. Kulingana na utafiti uliofanyika, kula zabibu katika siku za mwisho za ujauzito kunaweza boresha kupanuka na kulegeza kwa mlango wa uke.

Hitimisho

Comments