Umeambiwa kizazi kimeinama au kiko mbali....
Je, hata wewe umewahi kusikia kuhusu kizazi kuinama...!?
_____pengine ndugu, rafiki ama mke wako amefanyiwa vipimo na kugundulika kwamba kizazi chake kimeinama.
Kwa niaba ya aliyeuliza swali nimekuletea tafsiri nzuri ya kuinama kwa kizazi na jinsi gani inavoathiri afya ya uzazi kwa mwanamke.
Kuinama kwa kizazi kwa majina mengine ya kitaalamu tunawezakuita tilted uterus, retroflexed uterus, retroveted uterus au backward uterus ni namna mfuko wa mimba unapovutika kuelekea nyuma zaidi ya mlango wa kizazi badala ya kuvutika kuelekea mbele.
Mwanamke Mwenye Kizazi Kilichoinama huwa na dalili kama;
~Maumivu ukeni na nyuma kwenye mgongo wa chini wakati wa tendo la ndoa
~Maumivu kipindi cha hedhi
~Kupa changamoto kwenye kuweka pedi yako ili kuvyonza damu ya hedhi.
~Kupata maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI ) mara kwa mara
~Kushindwa kujizuia mkojo na
~Kuongezeka kwa eneo la chini ya tumbo.
Kumbuka siyo lazima kupata dalili zote kwa pamoja, kama unapata dalili zisizo za kawaida ni vizuri kufika hospitali ili kufanya vipimo ukaanza tiba mapema.
Nini Kinasababisha Kizazi kuinama?
Mfuko wa mimba ambao ndio kizazi tunachozungumzia ni sehemu tupu ambayo inajiweka katika eneo la chini ya nyonga za mwanamke.
Kazi yake ni kuhifadhi kichanga baada ya urutubishaji kufanyika.
Kizazi cha mwanamke kinaweza kuinama kutokana na sababu mbalimbali kama:
~Kulegea kwa misuli ya nyonga: mwanamke akishafikia kukoma hedhi au baada ya kujifungua, misuli inayosapoti tumbo la uzazi hulegea na hivo kupelekea kizazi kuanguka kwa nyuma.
~Kupanuka kwa kizazi kutokana na ujauzito, ama vimbe mbalimbali kama fibroids au vimbe ambazo ni saratani (tumor) zinaweza kusababisha kuinama kwa kizazi.
~Makovu ama msuguano kwenye nyonga
~Mfuko wa mimba ama kizazi kinaweza kupata makovu kutokana na hali mbalimbali mfano, maambukizi kama PID, uvimbe (endometriosis) ama makovu kutokana na upasuaji uliowahi kufanyiwa kwa kipindi cha nyuma. Makovu haya yanaweza kufanya kizazi kuvutika kuelekea nyuma.
Tiba Asili ambayo tunaiaminia sana kuweka kizazi sawa kama kimeinama ni Mizizi Ya Mbaazi.
Kwa kuchukua mizizi ya mbaazi mibichi ichemshe katika maji ya lita moja kwa muda wa dakika 15 kisha ipua acha ipoe iwe uvuguvugu chuja vizuri pima kikombe cha chai kimoja kunywa kabla hujala kitu asubuhi kila siku mara moja tu fululiza kwa siku 7.
Maji yakipungua unamwaga mizizi ya MMBAAZI unachuma mingine unaichemsha tena unaendelea na tiba hadi siku 7 kisha fanya check up uone hali itavyokuwa.
Mazoezi Mepesi Ya Kufanya Nyumbani Ili Kuinua Kizazi kama Kimeinama / Mazoezi Ya Kusaidia Kizazi Kisiinamie au Kulalia Upande.
👇
Zoezi la kwanza ni KNEE CHEST
Namna Ya Kulifanya
👇
Lala kwenye sakafu (unaweza kutanguliza kipande cha nguo). Mikono ikiwa imeshika kichwa, kunja goti mpaka ikaribie kugusana na kifua, fanya kama picha inaoeleza hapa chini. Tulia katika hali hiyo kwa sekunde 20 mpaka 30 kisha pumzika. Rudia zoezi husika mara 10 mapak 15 kwa kubadilisha miguu
Zoezi la Pili ni KEGEL au Pelvic Contraction
👇
Mazoezi haya yanalenga kuimarisha misuli ya nyonga.
Jinsi ya kufanya zoezi hili lala kwenye sakafu huku mikono yako ikiwa imenyooka kuelekea kwenye miguu. Taratibu nyanyuka eneo la katikati na makalio kuelekea juu kama picha inavyoonesha hapa chini.
Tulia ukiwa juu hivo hivo kwa sekunde 30 kisha pumzika (shusha kiuno chini sekunde kadhaa) rudia zoezi hili mara 10 mpaka 15 kwa siku. Unaweza kufanya mazoezi haya unapoamka au unapokwenda kulalal usiku maana hayahitaji pesa wala nguvu, ni utayari wako na mapenzi ya dhati juu ya afya yako.
"...Mungu akulinde na akuinue pale ulipokwama...."
________________ Endelea kujifunza na kuchukua hatua katika elimu nayokupa.... Hakuna kinachoshindikana ukiamua kuchukua hatua kila siku...
Barikiwa dr
ReplyDelete