JINSI YA KUREKEBISHA HOMONI NA CHANGAMOTO ZA HEDHI KWA KUTUMIA DAWA ZA ASILI

 


Wengi tumesumbuka na matatizo ya hedhi, kukosa ujauzito, kukosa hisia, matiti kujaa, kichefuchefu na mambo kibao ambayo tumekuwa hatuyaelewi, nina amini mpaka somo hili linaisha utajifunza mengi na utagundua mambo sio magumu kama unavyoyachukulia ila unachohitaji ni uelewa tu.

Ili uweze kunielewa huko mbeleni, ni muhimu kwa sasa uzitambue HATUA AMBAZO MWILI WAKO HUPITIA ILI WEWE UPATE HEDHI YENYE MPANGILIO au  UPATE UJAUZITO

1: Hatua ya kwanza, kwa msaada wa homoni ya FSH na Oestrogen yai hutengenezwa katika vifuko vya mayai (ovari)

2. Moja kati ya ovari huachia yai na kwa msaada wa homoni ya LUTEIN [LH] yai husafiri kutoka kwenye ovary mpaka kwenye mirija ya uzazi na kujishikiza likisubiri mbegu za mwanaume ili liweze kurutubishwa
   KAMA UTAKUTANA NA MWANAUME KWENYE SIKU ZA HATARI BILA KONDOMU
 3. Mbegu za mwanaume (shahawa) husafiri kuanzia kwenye mlango wa uke (cervix), kupitia tumbo la uzazi (uterus) hadi kwenye mrija wa uzazi, kulifikia yai la mwanamke lililopevushwa kisha hulirutubisha (kutengeneza kijusi)

4. Baada ya siku 14 au 21 Yai lililorutubishwa husafiri kupitia mrija wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi na kujishikiza na kuanza kukua siku hadi siku na huo ndio mwanzo wa safari ya ujauzito
KAMA HAUJASHIRIKI MAPENZI NA MWANAUME KWENYE SIKU ZA HATARI
   Iwapo yai la mwanamke halijarutubishwa katika siku za hatari, baada ya siku 14 hutolewa nje kama uchafu ambayo ndio damu ya hedhi tunayoipata kila mwezi

 Katika hatua zote hizo hapo juu tumeona vitu muhimu vinavyohusishwa ili kukamilisha mambo yote  ikiwepo HOMONI, MIRIJA YA UZAZI, OVARI (Vifuko Vya Mayai Ya Mwanamke), Fuko La Uzazi (Uterus) na MBEGU ZA MWANAUME.... hivyo ikitokea kuna tatizo katika moja ya vitu hivyo, kupata hedhi au ujauzito kwa wakati huwa ni jambo gumu, ndio maana umejiunga katika jukwaa hili kupata ufumbuzi wa haya mambo ili ukomboe muda, gharama na sintofahamu zote kuhusu uzazi....

Nimekuwa nikikutana na wanawake kama wewe waliokaa kwenye ndoa zaidi ya mwaka mmoja, mitatu na wengine mpaka miaka 7 bila kupata watoto ila baada ya kuwasilikiliza na kuwapa maelekezo juu ya mambo muhimu ya kuzingatia hivi sasa wanapata hedhi zao vizuri, wengine ni wajawazito na wengine wamejifungua tayari.






Baadhi Ya Shuhuda Ya Waliozingatia

Matokeo mazuri utayapata kikubwa ni wewe kuwa makini na kuchukua hatua, nina uhakika ndani ya siku 30 ni lazima uje na mrejesho mzuri tu.

Ili uweze kufanikisha ndoto ya kuwa na hedhi salama na kupata ujauzito ni lazima HOMONI zetu ziwe katika mpangilio ulio mzuri, hiyo ni lazima

Kwa tafsiri ya haraka haraka,
  Homoni ni kichocheo ambacho hutengenezwa na tezi mbalimbali mwilini na kusafirishwa kupitia damu kwenda sehemu inapohitajika mwilini ili kufanya shughuli maalum ya kibaolojia

Mfano: Homoni ya kike estrogen hutengenezwa na tezi iitwayo ovari na huenda kuchochea mambo mbalimbali kwa mwanamke kama kubarehe kwa mwanamke, kuleta hisia za kufanya mapenzi, kutoa ute, kukomaza yai siku za hatari n.k

Homoni zipo aina nyingi, kuna homoni za uzazi, usagaji chakula, zinazo ratibu matumizi ya wanga, mafuta na protein n.k katika somo letu hili tunajifunza homoni za uzazi kwa mwanamke pekee.

Homoni ambazo zinachochea matukio mbalimbali ya uzazi kwa mwanamke ni Oestrogen, Progesterone, Prolactin, Follicle stimulating hormone (FSH), Luteinizing hormone (LH), na Testosterone.

Homoni hizi huwa zinatengenezwa na ovari kwa mwanamke na kuratibiwa na (Anterior Pituitary Gland) tezi ambayo huhakikisha homoni zinabalansi isitokee homoni baadhi ziko juu na nyingine ziko chini.

Umuhimu wa kila homoni na madhara yake iwapo itapanda au kushuka sana.

Homoni ya Estrogen

👇🏾

~Homoni hii ikiwa katika ubora [kiwango chake sahihi] huchochea matendo yote wakati wa kubalehe kama Kuota matiti, Ngozi kuwa laini, sauti nyororo, nyoga kuongezeka, nyege, ute, yai kukomaa n.k
 IKIWA HOMONI HII IMEPUNGUA SANA AU KUONGEZEKA SANA
 Inaweza kukusababishia
~Shinikizo la juu la damu (presha kupanda)
    Hapa ndipo unakuwa unasikia hupumui vizuri, mapigo ya moyo yanaenda mbio, kuhisi joto jingi au kutoka jasho sana mara nyingi inapofika usiku, ukiona dalili hizi na hedhi yako haieleweki basi elewa homoni hii ipo juu sana kuliko inavyohitajika.

~Pili ongezeko la homoni ya oestrogen husababisha uwepo wa vivimbe katika fuko la uzazi kitaalam huitwa (fibroids)

~Tatu, unakuwa na nyege za hovyo yaani unasex huishiwi hamu hata usex kwa siku nzima nyege zipo tu
NA
~Iwapo homoni itakuwa iko chini sana, mwanamke utakuwa na tatizo la kukosa hisia za kufanya mapenzi hata uandaliwe vipi nyege hupati au zikija ni kwa mbaali halafu unakuwa na ukavu wa uke, ukishiriki tendo ni kama unabakwa maana ni michubuko na maumivu tu

~Oestrogen ikipungua hata hedhi unakuwa unapitiliza yaani unaweza kaa miezi hata mitatu huoni chochote, hata utege mimba siku zote za hatari hupati ujauzito

 Homoni nyingine ya muhimu ni Progesterone;
Hii Hutengenezwa na tezi ya dharura (corpus luteum) pale ambapo yai limetoka katika ovary
    ~Kazi yake kubwa ni kujenga ukuta wa uzazi ili kulea mimba inapotokea umebeba ujauzito, inaongezeka sana baada ya siku ya kupevuka kwa yai na baada ya mimba kutungwa.

~Mimba isipotungwa homoni hii inayoshikilia ukuta usibomoke hushuka kiwango chake na ndipo inawezesha ukuta kuporomoka kwa kutoa uchafu (damu ya hedhi) ili kwamba ukuta mwingine ujengwe upya kwa ajili mzunguko wa hedhi ujao

~Pia hukuza matiti wakati una mimba na kuendelea kufanya ukuta wa kizazi uwe imara ili mimba isichoropoke kabla ya miezi tisa

Homoni hii ikishuka sana hupelekea mimba kutotunga au mimba kuharibika kabla ya miezi tisa na homoni hii ikiwa nyingi kuzidi kiwango chake;
 ~Husababisha hedhi kutoka ikiambatana na mabonge
~Husababisha hedhi kutoka zaidi ya siku 7
~Husababisha maumivu makali wakati wa hedhi

Homoni  Ya Tatu ni Prolactin

👇🏾

Hii ni homoni ambayo hupanda sana wakati una mimba na wakati unakaribia kujifungua

~Hutengeneza maziwa yakutosha ili uweze kunyonyesha

~Huwa ina mkinga mama asipate mimba mapema akiwa bado ananyonyesha. Ukiwa unanyonyesha homoni hii huzalishwa kwa wingi na huzuia upevushaji wa mayai. Ila unashauriwa baada ya wiki sita tangu umejifungua kuwa makini maana kwa unyonyeshaji wa nadra kwa wanawake wengi unasababisha prolactin kutokuwa katika kiwango toshelevu kuzuia upevushaji wa mayai.
HOMONI HII IKIWA CHINI SANA husababisha kukosa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto kwa wanawake waliojifungua na HOMONI HII IKIWA JUU SANA husababisha mwanamke kutoa maji au maziwa hali ya kwamba huna mimba wala hunyonyeshi, chuchu kuuma,  maziwa kuvimba au kuuma

●Testosterone

Tunaita hii ni “homoni ya kiume” kwa sababu huwa ndio imetawala (inajionesha kuwa juu) kwa mwanaume kuliko homoni zingine. Lakini wanawake pia huwa wana hii homoni katika kiwango kidogo sana. Wao homoni inayotawala ni oestrogen.

~Homoni hii inasaidia sana uhifadhi wa mafuta mwilini, pia inasaidia katika utumiaji wa vyakula vya mafuta, protini na wanga, pia inasaidia sana kutengeneza misuli ya mwili wako. Hivyo ni ya muhimu pia kwa mwanamke japo sio muhimu sana… HOMONI HII IKIZIDI KWA MWANAMKE hupelekea mwanamke kuwa na dalili za vivimbe katika vifuko vya mayai [PCOS], kuote ndevu au manyoya sehemu za kifua, sauti kuwa ya kiume n.k zaidi ni mwanamke kukosa mimba kwa sababu ya ovary zake kushindwa kuzalisha mayai yenye afya

Follicle Stimulating Hormone (FSH)

👇🏾
Hii ni homoni ambayo inakomaza mayai, na huanza kupanda kwenye damu siku ya kwanza tu umeanza kuingia hedhi.

 Yenyewe inaanza kuandaa yai ambalo litapevuka siku ya hatari katika mzunguko wako. 

Homoni ya Lutein (LH; Ni homoni ambayo husaidia yai liweze kutoka kwenye ovari, liende kwenye mirija ya uzazi kwa ajili ya urutubishaji.

Mpaka hapa umeweza kutambua ni homoni gani inakusumbua kulingana na dalili unazozipata?

Kama umegundua kuwa unalo tatizo la mvurugiko wa homoni bila shaka utakuwa unajiuliza kipi kinasababisha homoni zako kuvurugika, Kipi ukifanye ili uweze kuziepuka hizi kero za homoni, hedhi na kupata ujauzito.

Yote nimekuwekea hapa:

Moja ya jambo linalovuruga homoni zako ni MAGONJWA

Mfano

👉🏾Mtu mwenye matatizo ya Kisukari moja kwa moja ana uwezekano wa kupata matatizo ya homoni kuvurugika kwa sababu ya matatizo yake ya insulin kushindwa kuratibu kiwango cha sukari na wanga katika damu, kama una matatizo ya kisukari bila shaka utakuwa chini ya uangalizi wa madaktari... Kundi la watu wa kisukari sio kubwa kwa hapa Tanzania, wengi wetu homoni zetu zimevurugika kwa sababu ya;

•Jambo la Pili ni Matumizi ya Njia Za Kisasa Za Uzazi wa Mpango.

==> Ukiachana na propaganda za serikali na mambo ya uchumi umewahi kuwaza na kutafakari ni kwa nini haswa huwezi kubeba mimba ukiwa unatumia uzazi wa mpango?
   Dhamira kuu ya njia za kisasa huwa ni kuua au kuharibu uwezo wa uzalishwaji wa vichocheo au homoni  za uzazi (progestrone & oestrogen) ili mimba isifanikiwe kutungwa.

Unapo maliza kutumia njia za uzazi wa mpango na mwili wako ukashindwa kuupa vyakula bora, mwili huendelea kuwa duni na kuendelea kuzoea hali ya uzalishwaji duni wa homoni zako hivyo kujikuta unakuwa na changamoto sugu za hedhi kuvurugika kiasi hata ukijaribu kupata mtoto mwingine mambo huonekana kuwa magumu, UNATAKIWA MWILI KUUPA LISHE YA NGUVU MFULULIZO WALAU KWA MWEZI MMOJA MARA TU BAADA YA KUMALIZA KUTUMIANJIA ZA UZAZI WA MPANGO, hapo chini utaona namna ya kuandaa tiba lishe

    Kesi za mara kwa mara ambazo unaweza kuzisikia kwa wanaotumia au waliowahi kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango ni pamoja na..

~Hedhi kusimama hata miezi miwili au zaidi bila kupata hedhi, au hedhi kutoka mfululizo au kutoa matone ya damu mara kwa mara hata siku zisizokuwa za hedhi

~Matiti kujaa sana kabla ya hedhi, kuhisi maumivu makali ili hii hutegemea na njia ipi ya kisasa unayotumia au uliyowahi kutumia kupanga uzazi.....

•Sababu nyingine inayovuruga homoni ni Maambukizi Katika Via Vya Uzazi

~Maambukizi ya Bakteria au Fangasi katika via vya uzazi huathiri mpangilio wa homoni, hii ni kwa sababu bakteria au fangasi huweza kusambaa kwenye fuko la uzazi, mirija ya uzazi na kushambulia fuko la mayai (ovari). Fangasi au bakteria wanaposhambulia husababisha ovary kuwa na vivimbe vidogo vidogo (ovarian cyst) jambo ambalo matokeo yake husababisha ovary kushindwa kuzalisha mayai ya mwanamke kwa wakati na kupelekea kukosa hedhi kwa wakati sahihi. Dalili nyinginezo zinazoweza kuonesha kuwa una mashambulizi ya bakteria au fangasi ni maumivu makali kwenye nyonga, maumivu ya pembeni mwa tumbo maeneo ya chini ya kitovu, mkojo kuwa mchafu au U.T.I sugu, Kutokwa na Uchafu Ukeni na kama umepima hospital unaweza kuambiwa una tatizo la P.I.D

Jambo jingine linalovuruguka homoni za mwanamke ni matumizi ya vidonge vya dharura vya kuharibu mimba kama P2, mesoprostol na kuharibu mimba mara kwa mara kwa njia za kumeza madawa makali.

•Kuwa na matatizo ya Uvimbe katika Fuko la Uzazi (Fibroid/Myoma)

Mwenye tatizo hili huwa na dalili km kutoka hedhi nyingi kupitiliza, unaweza kupata hedhi zaidi ya siku 7 au ikatoka mara mbili kwa mwezi

~Kuhisi km kitu kinacheza tumboni au km kimening'inia tumboni

~Tumbo kuonekana kujaa

~Maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu n.k (tutajifunza haya kesho kutwa)

Ni jambo gani kati ya hayo niliyotaja umewahi kuyapitia, kuyatumia au unahisi ndio chanzo cha wewe kukosa mimba na hedhi kuvurugika..!?

Mambo Ya Kuzingatia na Dawa Asili za Kusaidia Kutibu Tatizo La Mvurugiko wa Homoni (Hormones Imbalance

Hapa nimekuandikia njia ambazo nimewashauri watu wenye changamoto kama yako na wamefanikiwa;

○  Katika njia hizi  ichague mojawapo ambayo unaweza kuiandaa, fuatisha vipimo vyake na itakusaidia kukupa matokeo mazuri...

Njia ya Kwanza ni Kutumia ASALI Mbichi ya Nyuki Wadogo kwa kuchanganya na VIUNGO VYA MAPISHI.

~Hii ni njia ya asili ambayo huwasaidia haswa wale ambao mvurugiko wao wa homoni umesababishwa na uzito kuwa juu, mimba kuharibika au matumizi ya muda mrefu ya njia za uzazi wa mpango kama kijiti na sindano.

Mahitaji:
>Tangawizi kubwa nne (katakata ili iweze kusagika vyema kwenye blenda au twanga) kama ni unga basi iwe vijiko nane

>Vitunguu saumu glass moja (menya vizuri) kama ni unga iwe vijiko nane hadi kumi

>Mdalasini wa unga vijiko sita

>Asali mbichi PURE ya nyuki wadogo lita moja. [ikikosa ya nyuki wadogo unaweza kutumia asali ya nyuki wakubwa kama hausumbuliwi na vidonda vya tumbo, muhimu iwe asali mbichi]

Maandalizi.

Chukua tangawizi na vitunguu saumu na usage kwenye blenda viwe laini kisha utaweka unga wa mdalasini na utaanza kumimina asali yako kidogo kidogo hadi iishe kisha itakuwa nzito sana hivyo utaanza kuongeza maji kidogo kidogo hadi nusu lita ya maji iishe kabisa kwa maana juisi yako itakuwa ujazo wa lita moja na nusu

>>Kama viambata vyote vitakuwa vya unga au umesaga kwa kinu, huna haja ya blenda, utaweka viambata vyote muhimu kwenye kifaa cha kukorogea iwe sufuria au kontena kisha utaanza kuweka asali na kumalizia na maji nusu lita ya maji ya kawaida.

•Matumizi ya dawa
    >>Asubuhi utatumia nusu glass ya juisi hii, mchana na jioni hadi itakapoisha, mathalani itachukua siku tano kuimaliza, utaandaa nyingine tumia dawa hii mfululizo kwa siku 15 hadi 21.

Utapona na usisahau kuniletea mrejesho wako; 

02: Njia Ya Pili ni Dawa Nne Za MITISHAMBA

Njia ya pili ni kutumia dawa za mitishamba na huku ndipo mirejesho mingi inakuwa na majibu mazuri kwa wenye changamoto nyingi za uzazi yatokanayo na U.T.I sugu, Uzazi Wa Mpango,  Vivimbe n.k

Chukua Dawa Asili hizi nne katika ujazo unaolingana.

👇

Unga wa Mrehani [basil leaves powder] robo kilo

Unga wa habat sawda (black seed), robo kilo

Unga wa mbegu za uwatu (fenugreek) robo kilo na Unga wa mizizi ya Mkunde pori robo kilo. [viungo hivi vinapatikana maduka ya tiba lishe]

MAANDALIZI
   Changanya kwa pamoja dawa hizi kwenye bakuli moja, uwe unatumia unga wa mchanganyiko wa dawa hizi kijiko kidogo kimoja kwenye chai, uji, au maji moto tumia mara tatu kwa siku, kwa wiki 3 mpk 4. Kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu utakuwa umefanikiwa kutatua hizi changamoto za homoni kuvurugika na kama ni kuhusu kupata mimba inakuwa rahisi sana

Haijalishi ni kwa muda gani umekuwa ukitafuta suluhu bila mafanikio, kama utaamua kuanza upya na kuchukua hatua, utaona matokeo mazuri, natumaini utanipa mrejesho wako pia kadri utavyokuwa unaendelea kutumia

Ili uweze kupata matokeo mapema itakuwa vyema kama utajitahidi kujiweka vizuri kwenye upande wa vyakula, kama tujuavyo kuwa unachokiingiza mwilini ndicho kina nguvu zaidi ya kukujenga au kukuharibu hivyo hakikisha unakula vile vyenye kuupa mwili afya njema zaidi

• Punguza (ikibidi acha) kula vyakula vya kukobolewa kama mkate mweupe, chapati, mandazi n.k kama unapenda sana ugali basi tumia dona, kama ni mkate tumia ile mikate ya brown, tumia nafaka ambazo hazijakobolewa

• Pendelea zaidi kula matunda kwa wingi mfano ndizi mbivu, papai, chungwa, embe, nanasi, karoti, tikiti, tango n.k (matunda utayopata kula) na mboga za kijani kwa sana tu. (matunda na mboga za kijani iwe sehemu ya mlo wako pia)

Kuna viungo vya chai / mapishi ambavyo nakushauri kuvipa kipaumbele zaidi mfano Iliki, Mdalasini, Tangawizi, Karafuu na  Binzari Ya Manjano, Kotimiri na Mrehani

Ni viungo vizuri kwa kusafisha njia za mkojo, damu na kubalansi homoni iwe kwa mwanaume au mwanamke....

Hakuna kilicho kigumu hapa kama utaamua kuchukua hatua juu ya kile ambacho nimekufundisha na nina uhakika utakuja kunipa mrejesho ulio mzuri

Kama unahitaji dawa bora na asili iliyoandaliwa, nakushauri kuitafuta MIXED HERBS POWDER 

Ni dawa lishe ambayo imeandaliwa kwa mchanganyiko wa dawa asili za uzazi ambayo

✓ Inakusaidia kusafisha via vya uzazi yaani inasafisha mira ya uzazi na fuko la uzazi ili kuondoa majimaji au uchafu na fangasi

✓ Inaondoa makovu na vivimbe kwenye fuko la uzazi, mirija na kwenye vifuko vya mayai (fibroids, scars and ovarian cyst)

✓ Kwa kuwa imechanganywa na mrehani ndani yake, dawa hii inakusaidia pia kuondoa changamoto ya mvurugiko wa hedhi kwa wale ambao mnapata tatizo la kukosa hisia, kuwa wakavu ukeni, period kupishana, damu ya hedhi kuwa na utelezi, mayai kutokupevuka n.k....

DOZI HII YA UZAZI, NAKUPA KWA TSH 66,000 tu POPOTE ULIPO

....hakuna gharama ya usafirishaji (free delivery)

Ninapatikana Machinga Complex, KARUME (Dar) na mkoani natuma kwenye Bus

Kwa ufafanuzi zaidi chukua namba yangu 0763872652 NITAKUSAIDIA KUKUELEZEA  AMBAPO HUJAELEWA

Comments

  1. Thanks Dr nmejiunga wiki hii na nmejidunza mengi nliyokuwa siyajui pia mm Ni muhanga mkubwa wa matatizo haya nitayafanyia kazi nitaleta asanteeemrejesho mungu akubarik san

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shukrani sana mpendwa. Karibu sana na Mwenyezi Mungu akupe uponyaji

      Delete
  2. Thanks Dr nmejiunga wiki hii na nmejifunza mengi nliyokuwa siyajui pia mm Ni muhanga mkubwa wa matatizo haya nitayafanyia kazi nitaleta mrejesho asanteee mungu akubarik san

    ReplyDelete
  3. Asante Sana doctor nimejifunza vitu vingi Sana barikiwa Sana.

    ReplyDelete
  4. Je vitu hivyo kama unga wa kuchanganyia vinapatikana wap kwa hapa dar es salaam

    ReplyDelete
  5. 🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

    ReplyDelete

Post a Comment