MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UTAFUTA UJAUZITO

Hakuna siku tutaishi bila kuwa na changamoto, kwa sababu sisi wanadamu tunawekewa vikwazo ili tukue kiakili na kujua thamani ya kile tunachokitafuta.

Maisha yangekuwa kama kamali basi yasingekuwa na thamani hata kidogo,,,

Kupakata mtoto, kuwa na idadi ya watoto unaowataka inawezekana vizuri tu.

Endelea kutafuta tiba, endelea kuimiliki ndoto yako, haijalishi utaachwa na wanaume wangapi kwa sababu ya kukosa mtoto, fungu lako lipo na kuzaa inawezekana....

Haijalishi mawifi na wakwe zako watatutakana kiasi gani, haijalishi dunia itakukandamiza mara ngapi kama hujafa basi iambie nafsi yako kuwa hili litapita tu nami sintoacha kupambania ndoto yangu maana Inawezekana....

• Tafuta mazingira yenye kukuhamasisha, kukupa utulivu wa akili, ambatana na watu sahihi ambao watakupa majibu ya maswali yako km daktari, tabibu au hata yeyote mwenye uelewa wa elimu ya uzazi hakika ITAWEZEKANA TU.

 Jambo Moja Ambalo nakushauri kutolisahau ni Kanuni Bora za Ulaji.

👉 nakubainishia chakula kipi upendelee kula ili kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito au kuimarisha afya ya ujauzito kwa ujumla..

👉  Baada ya kusoma orodha hii, nina uhakika utagundua wapi unakosea katika vyakula vyako, utafanya marekebisho na ndani ya mwezi wa pili utanipa mrejesho wako.

👉 Kwa mwanamke anayetafuta ujauzito vyakula unavyopaswa kula ni vile vyenye folic kwa wingi. Chakula kina mchango mkubwa linapokuja suala la kupata ujauzito.

👉 Unatakiwa ujuwe unakula nini na kwa ajili ya nini, usile tu bora ushibe, hiki ndicho kimefanya wengi kutofanikiwa.

👉 Kula mafungu ya vyakula yafuatayo ili kuimarisha afya yako ya uzazi na homoni kwa ujumla:

1. Chakula cha mwanamke anayetafuta ujauzito hakikosi Mboga za Majani na Matunda.

Matunda.

👉 Ili kujiongezea nafasi ya kupata ujauzito, ili kuwa na mayai yenye ubora hakikisha sahani yako ya chakula imejaa matunda na mboga za majani.

👉 Hakikisha nusu ya ujazo wa chakula unachokula kwa siku imebeba matunda na mboga za majani.

👉 Matunda matatu muhimu zaidi kwa ajili hii ni ndizi, parachichi na tikiti maji.

👉 Matunda haya yanafanya utengeneze mayai bora kwa afya ya uzazi na yanasaidia pia kusafisha mwili wote ikiwemo mji wa uzazi.

Hakikisha matunda yote haya matatu unakula kila siku.

👉 Unahimizwa pia kula mboga za majani nyingi na za kutosha kila siku. Unaweza pia kutengeneza juisi freshi ya mboga hizi za majani ili kupata viinilishe kwa kiwango cha juu kabisa.

2. Mafuta mazuri

👉 Unahitaji mafuta bora ili kuwa na afya bora ya uzazi. Mafuta ninayohimiza hapa ni yale yatokanayo na mimea kama vile mafuta ya zeituni, mafuta ya parachichi, mafuta ya nazi, mafuta ya mbegu za maboga na mafuta ya karanga.

👉 Mafuta haya husaidia kutibu na kuzuia uvimbe kwenye uzazi (mwili), kuweka sawa mzunguko wa hedhi, kuweka sawa homoni na uzazi kwa ujumla.

3. Wanga unaomeng’enywa pole pole.

👉 Utahitaji pia kula vyakula vyenye wanga lakini wanga ule ambao humeng’enywa pole pole na mwili (complex carbs).

👉 ACHA VYAKULA VYENYE SUKARI NYINGI au VILIVYOKOBOLEWA.

Madhara ya vyakula vya kukobolewa au vyenye sukari nyingi   kama soda, biskuti, keki, mkate mweupe na wali mweupe humeng'enywa kwa haraka sana na sukari hubadilishwa kuwa glukozi kwenye damu (damu sukari).

👉 Ili mwili uweze kuiondoa hii damu sukari kwenye damu kongosho huongeza insulin kwenye damu na tafiti zinaonyesha kiasi kingi cha insulin kwenye damu yako kinasababisha kuvurugika kwa homoni hivyo zoezi la kutunga ujauzito huwa gumu kwa walaji wa milo yenye sukari nyingi au kukobolewa

👉 Wanga mzuri ni ule wenye nyuzinyuzi nyingi (fiber) kama vile mkate ambao unga wake haujakobolewa (brown bread), ugali wa dona, maharage, matunda, mboga za majani.

👉 Vyakula vya wanga vya namna hii vina matokeo mazuri kwa damu sukari (kisukari) na insulin.

👉👉🏾 Basi robo ya chakula chako unachokula kiwe ni aina hii ya vyakula vya wanga mzuri.

4. Protini

👉 Punguza sana kula nyama nyekundu na ule zaidi samaki hasa samaki wa baharini.

 Kula zaidi kuku wa kienyeji, mayai ya kienyeji, bata na nguruwe (kama dini inakuruhusu).

👉 Vyakula hivi ni vyanzo vizuri vya protini nzuri, madini ya zinki na madini ya chuma vitu ambayo ni muhimu kutafutia ujauzito wenye afya.

👉 Samaki anajulikana kama Samoni (salmon kwa kiingereza) ni samaki mkubwa mwenye mnofu mwekundu ambaye ni samaki wa maji baridi na dagaa ni samaki wazuri kula kwa mtu anayetafuta ujauzito.

👉 Samaki wanasaidia kukupa mafuta mazuri (omega 3), wanatengeneza mfumo wa neva wa mtoto na kuzuia ujauzito usitoke kirahisi.

👉 Samaki napendekeza wale wa hapa hapa kwetu Tanzania kwani ndiyo wanavuliwa kwa namna nzuri kiafya na hawana madawa mengine yanayotumika kuwahifadhi wasiharibike ambayo yanaweza kuwa na madhara kwa mtumiaji.

👉 Kula Mayai mawili kama unaweza kula kila siku. Mayai hayaongezi uzito kama ambavyo wengine wanasema bali husaidia kukufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu na hivyo kukusaidia usile mara kwa mara jambo linalopelekea usiwe na uzito mkubwa.

👉 Kama upo bize kupata protini nzuri basi nakusihi vyanzo vyake zaidi viwe ni vile vinatokana na mimea kama maharage, choroko, dengu, karanga, mbegu za maboga na mbegu mbegu nyinginezo.

5. Maziwa na Bidhaa zake

👉 Kama uwezo wako unaruhusu, pata kikombe kimoja cha maziwa mtindi au fresh kila siku hakikisha yawe ni asili au hata ukitumia Tanga Fresh vipimo vyao viko vizuri. Maziwa sio lazima sana ila kama unaweza kuyapata yatumie.

•Epuka matumizi ya kahawa, kama ni mpenzi wa kuandaa uji au chai viungo kama soya, iliki, mdalasini, karafuu, tangawizi, tende, ulezi ni viungo vizuri pia kuandaa katika vinywaji vyako.

Ukiweka katika mpangilio mzuri kama hivi walau kwa wiki 3 hadi 4 matokeo utayopata utakuja kushea nami mwezi ujao.

Kama una changamoto nyingi za uzazi zinazokusumbua, tumia
MIXED HERB POWDER

➡️Ni dawa asili ambayo inaondoa uchafu na fangasi kwenye kizazi

➡️inatoa uvimbe kwenye kizazi (fibroids) na vimbe kwenye fuko la mayai (ovarian cysts)

➡️ Inazibua mirija na kuondoa tatizo la mvurugiko wa homoni kama unakoswa hisia, ute, mimba hazinasi na hedhi haieleweki

Dozi hii unaipata kwa Tsh 66,000 tu

Wakazi wa Dar, tupo Machinga Complex na pia tunakuletea hadi ulipo FREE

Kwa mawasiliano zaidi tutafute 0757487684

Asili Yetu Afrika
Tunatimiza Ndoto Yako Ya Uzazi


Comments