JINSI YA KUZIBUA MIRIJA YA UZAZI KWA KUTUMIA NJIA ASILI

Umepima na ukaambiwa mirija imeziba? au Unahisi Nyonga kupata Maumivu!
Unamfahamu ndugu yako mwenye tatizo la mirija ya uzazi kuziba?

Katika somo hili nitakuelekeza namna ya kuweza kutumia njia asili kuhakikisha unazibua mirija, kutoa uchafu na makovu katika mirija ya uzazi

 ▪︎Mirija ya Uzazi (fallopian tubes) ni mirija miwili myembamba inayokuwa katika tumbo la uzazi, mrija mmoja upande wa kulia na mrija mwingine upande wa kushoto, mirija hii hulisaidia yai lililopevuka liweze kusafiri kutoka katika mfuko wa yai (ovary) mpaka kwenye kifuko cha uzazi katika kipindi cha siku za upevushaji (ovulation days/danger days)

 

👉🏾 Kitu chochote kinapojitokeza na kuzuia yai la mwanamke lisiweze kusafiri kutoka kwenye fuko la mayai (ovari) mpaka kufika kwenye kifuko cha uzazi (uterus), humfanya mwanamke kukosa kubeba mimba.

 ~hali hii ya mirija kuziba isipotibiwa mapema hukufanya kukosa mtoto (ujauzito) sababu yai hushindwa kufika kwenye mfuko wa uzazi kwa wakati sahihi kwa ajili ya upevushaji... Kuziba kwa mirija huweza kuliharibu yai kabla halijafika kwenye fuko la uzazi iwapo kama mirija ina maambukizi ya fangasi/bakteria au maji machafu pia huzuia mbegu za mwanaume kufikia yai lilipo unaweza kubaini mirija ina shida iwapo kama shahawa za mwanaume zinatoka nje ya uke dakika chache (5-10) mara baada ya kumwagwa ukeni (kupiiz mnaita)

Mambo yeye kukusababishia mirija yako ya uzazi kuziba, kuwa na vivimbe au kujaa maji!?

1. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile Pangusa, kisonono, kaswende, n.k

2. Utoaji mimba (Abortion) wa mara kwa mara kwa njia za kienyeji

3. Magonjwa ya maambukizi kama vile U.T.I sugu na Fangasi (P.I.D)

4. Hali ya kukua kwa uvimbe aina ya fibroid ambayo hupelekea kuziba nafasi ya mirija ya uzazi

5. Mimba kutunga nje ya kizazi na kusababisha upasuaji hali ambayo hupelekea michubuko au majeraha kwenye mirija ya uzazi ambayo hupelekea mirija kuvimba na kuziba

6. Hali ya kukua kwa uvimbe aina ya fibroids ambayo hupelekea kuziba nafasi ya mirija ya uzazi

Unaweza kubaini kama mirija yako imeziba mapema tu kwani huwa kunakuwepo na dalili za wazi kama vile;

1. Kutokwa na uchafu kama maziwa sehemu za uke na mara nyingi uchafu huu huwa na harufu ya kisamaki

2. Mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy)

3. Maumivu makali ya nyonga katika siku za hatari na maumivu makali mno wakati wa hedhi

4. Maumivu ya kiuno ama tumbo la chini mara kwa mara.

5. Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa au hata wakati wa kukojoa

 

Unafanyaje kuzibua mirija ya uzazi, kuondoa uchafu na kuhakikisha tunakuwa salama?
     ...haya matatizo ya uzazi yasikupe hofu kwa sababu yanatibika. Kwanza kabisa Muamini Mwenyezi Mungu kuwa hali uliyonayo kwa sasa ni ya muda tu na utavuka salama... 

Pili, ili kuzibua mirija, kusafisha njia ya uzazi na kuweka homoni zako inahitaji kujiweka vizuri katika ulaji na unywaji wako:-

👉🏾 Vyakula vizuri vya kucheza na navyo katika mapishi na milo yako ni pamoja na binzari ya manjano, pilipili, tangawizi, limao, karafuu, maziwa mtindi, ukwaju, vitunguu aina zote, mdalasini na siki ya tufaa (apple cider vinegar), kotimiri (parsley) hivi ni vyakula ambavyo ni vizuri haswa katika kusafisha njia ya uzazi na kuondoa vimbe au maji katika mirija na fuko la uzazi.

Simaanishi kuwa ni lazima ule au unywe vitu hivyo vyote kwa pamoja la hasha.! Nachomaanisha ni jitahidi kuvitumia mara kwa mara haijalishi umepata vingapi hata kama ni viwili au vitatu kati ya hivyo kwa siku ni sawa tu

Kuhusu mmea mzuri na rahisi kuupata kwa ajili ya kuzibua na kusafisha mirija kama imejaa maji ni Mizizi ya Mbaazi....

 Namna Ya Kuitumia ni rahisi sana, CHUMA MIZIZI KIASI, (ioshe) KISHA CHEMSHA KWENYE KIASI CHA MAJI, ikipoa weka kwenye kikombe kimoja kidogo cha chai na unywe asubuhi, mchana na jioni. kama huna muda mchana Tumia Asubuhi na Usiku kwa Wiki 12 utarudi hospital kupima mirija yako.

Wakati unatumia dawa hii ya mizizi ya mbaazi ni vyema mgonjwa uwe umeshakula na kushiba kabla ya kunywa dawa hii ili isikuzingue kichwa maana ina nguvu

Njia Nyingine Ya Pili kwa wale mlio karibu na vijiji ni Mizizi Ya Mgomba na Mizizi Ya Muembe

MAHITAJI  ;

i. Bakuli moja Kubwa la Mizizi ya Muembe.

 ii. Bakuli Moja kubwa la Mizizi ya Mgomba.

 iii. Maji safi na salama kiasi cha lita tatu.

UANDAAJI
   Chukua mizizi ya muembe, changanya na mizizi ya mgomba, weka kwenye sufuria kisha ongeza maji safi na salama kiasi cha lita tatu halafu chemsha mpaka mchanganyiko utakapoanza kutoa supu.

 Chukua supu yako na uihifadhi kwenye chupa au dumu

MATUMIZI:
     
Tumia glass moja ya dawa yako, mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni kwa muda wa siku14 uone mabadiliko

 Kama huwa unabeba ujauzito halafu unatoka wenyewe, dawa hii pia husaidia sana kuimarisha fuko la uzazi na kubalansi homoni ya progestrone inayoshikilia ujauzito usiachie kabla ya miezi tisa.

Wewe kama mwanamke,kwa usalama wa mirija ya uzazi na afya ya uzazi kwa ujumla;-
    ~Acha au Punguza kabisa vyakula vya kutiwa sukari nyingi na vile vya kukobolewa kama magonjwa ya uzazi yanakuandama mara kwa mara.

*Jitahidi kuwa mtu wa kula vyakula visivyotiwa mafuta mengi na hii itakusaidia mwili kutokuwa na mafuta mengi (chorestrol) kuzidi

~Ulaji wa matunda na mboga ni muhimu kwa ajili ya kila mwanamke kwani husaidia kubalansi homoni za mwili iwapo mzunguko wako wa hedhi haueleweki.

~Jilinde dhidi ya magonjwa ya Zinaa, P.I.D au Fangasi na Matatizo Ya U.T.I (yutiai) nadhani somo lililopita tulielewana vizuri kuhusu kutibu
kama unasumbuliwa na Fangasi, P.I.D na U.T.I na unahitaji kujtibu bofya Jitibu Fangasi, U.T.I na P.I.D sugu

Chagua njia mojawapo unayoiona ni rahisi kwako... Njia hizi hazihitaji gharama kubwa sana.. ni muhimu kuwafundisha na wengine, ninaamini kama tutashirikiana kupeana mwongozo, tukaelezekana tiba na kupeana mwanga juu ya matatizo haya ya uzazi basi tutaepuka kutapeliwa na kupunguza gharama kubwa za madawa na oparesheni...

Ninaamini baada ya wiki mbili kama utazingatia masomo ya kwenye blog hii, utakuwa umefanikiwa Insha'Allah.

Kama umehangaika kuhusu uzazi na unahitaji nikusaidie kutatua changamoto hizi kwa ushauri na dawa
Nitafute kwa Kupiga Simu / WhatsApp namba 0757487684

Karibu AsiliYetuAfrika

Tunazo dawa kwa ajili ya;
~ Kuondoa Uvimbe katika fuko la Uzazi na kwenye Vifuko Vya Mayai
~Kuondoa Fangasi kwenye kizazi na Kuzibua Mirija
~Kutibu Tatizo la Mvurugiko wa Homoni, Hedhi kwa wasiopata Ute wa Uzazi, Hisia na Kukosa Kubeba Ujauzito au Mimba Kuharibika
pia Ipo Dawa Asili kwa Wanaume wenye Matatizo ya Manii na Nguvu Za Kiume kwa Ujumla




Tuandikie Changamoto Yako Kwenda WhatsApp namba 0757487684

Comments