Jinsi Ya Kutuliza Maumivu Ya Tumbo katika Siku za Uzazi / Siku Za Hatari

Baadhi yetu kina mama hupitia hali ya kuhisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu au kwenye kinena siku za katikati ya mzunguko yaani katika siku za upevushaji wa yai...

Nini kinasababisha upate hali hii…..!

Kikawaida kwa wanawake wengi yai huanza kuachiliwa kuanzia wiki 2 (siku 14) tokea kuanza kwa hedhi...

Mabadiliko ya homoni yanayotokea kipindi hiki huchochea vifuko vya mayai (ovaries) na kupelekea kufanya yai lililokomaa kupasua utando unaolizunguka ili liachiliwe kutoka kwenye mfuko wa yai  (ovari). Yai hili hutoka na majimaji yaliyokuwa yanalizunguka na pia damu pia.

Kitendo cha yai kupasua utando ili litoke hupelekea maumivu kidogo ya tumbo kitaalamu hujulikana ka mittelschmerz

Pia majimaji yanayotoka pamoja na yai kutoka kwenye ovari yanaweza kusababisha kuta za mirija ya uzazi (fallopian tubes) kupata michomo (inflammations) na kupelekea kupata maumivu haya.
     Dalili zake ni pamoja na maumivu mithili ya kichomi au tumbo kukaza sehemu ya chini ya kitovu. hali pia inaweza kuambatana na kuona damu kidogo ukeni (spotting)

Hali hii huisha ndani ya siku 1 hadi mbili na sio zaidi ya hapo.

Maumivu haya huwa ni ya kawaida hayapaswi kuathiri shughuli zako za kawaida, IWAPO UNAPATA MAUMIVU MAKALI au vitone vya damu vinaendelea kutoka zaidi ya siku mbili ni vyema kufika hospital kwa uchunguzi zaidi.

UFANYE NINI KUTULIZA MAUMIVU HAYA.

1. Kanda tumbo sehemu ya chini ya kitovu na maji ya moto inasaidia kuondoa/kupunguza hali hii au unaweza kuoga maji ya uvuguvugu

2. Tumia vyakula vinavyosaidia kuondoa maumivu ya misuri kama mdalasini, tangawizi, pilipili, kitunguu, komamanga, mafuta ya samaki, maharage ya mbaazi n.k husaidia kupunguza maumivu katika mwili.

3. Chai ya Majani Ya Mnanaa.

Kwa wanawake ninaowahudumia na kuwashauri katika mambo ya uzazi, chai hii imekuwa msaada wako.
Unaandaa chai yako  ya iliki, mdalasini, tangawizi na karafuu kisha wakati umeweka kwenye kikombe chako unachukua majani kadhaa ya mnanaa (mint leaves) unatia kwenye kikombe chako na kunywa. Mnanaa una harufu nzuri katika chai pia hupoza maumivu ya tumbo katikati ya mzunguko. Unaweza kuwekea na limao kidogo ukitaka

Muhimu Wewe Kama Mwanamke EPUKA:

👉🏻 Vyakula au Vinywaji Vyenye Kutiwa Sukari Nyingi kama Soda, Ice Cream n.k

👉🏻 Vyakula vya kukobolewa kama Ugali Sembe, Mkate Mweupe.

👉🏻 Punguza kula Vyakula vya Kutiwa Mafuta mengi mfano Chipsi, Nyama za Ku-roast n.k

ZINGATIA SANA;
👉🏻 Matunda, Mboga Za Kijani na Maji walau lita Moja kwa Siku
~Pendelea sana kutumia Iliki, Kotimiri, Vitunguu, Tango, Parachichi, Bamia, Karoti, Tangawizi, Papai, Msusa (Majani Ya Maboga), Mdalasini, Asali mbichi, Apple, Mbegu za Maboga kutaja machache.

Kama umekuwa ukisumbuliwa na changamoto za uzazi kama Uvimbe, Mvurugikowa Hedhi, Fangasi sugu,mirija kuziba au kizazi kuwa na uchafu na ungependa kujiweka vizuri.

Wasiliana nami uniambie ni jambo gani linakusumbua ili nikupe njia asili ya kukusaidia kulitatua
Piga simu /WhatsApp 0757487684


Makala unazoweza kuzisoma tena
MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUFAHAMU KUHUSU HOMONI, HEDHI NA KUPATA UJAUZITO

NJIA ASILI ZA KUTIBU FANGASI, U.T.I sugu na P.I.D

Comments